Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 37:5-17 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako;mtumainie yeye naye atafanya kitu.

6. Ataufanya wema wako ungae kama mwanga,na uadilifu wako kama jua la adhuhuri.

7. Tulia mbele ya Mwenyezi-Mungu, mngojee kwa saburi;usihangaike juu ya wale wanaofanikiwa,watu wanaofaulu katika mipango yao mibaya.

8. Epuka hasira wala usiwe na ghadhabu;usihangaike maana hiyo huzidisha ubaya.

9. Watu watendao mabaya wataangamizwa,bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi.

10. Bado kitambo kidogo, naye mwovu atatoweka;utamtafuta pale alipokuwa, wala hutamwona.

11. Lakini wapole wataimiliki nchi,hao watafurahia wingi wa fanaka.

12. Mwovu hula njama dhidi ya mwadilifu,na kumsagia meno kwa chuki.

13. Lakini Mwenyezi-Mungu humcheka mwovu,kwani ajua mwisho wake u karibu.

14. Waovu huchomoa panga na kuvuta pinde zao,wapate kuwaua maskini na fukara;wawachinje watu waishio kwa unyofu.

15. Lakini panga zao zitawapenya wao wenyewe,na pinde zao zitavunjwavunjwa.

16. Afadhali mali kidogo ya mtu mwadilifukuliko utajiri wa watu waovu wengi.

17. Maana nguvu za waovu zitavunjwa,lakini Mwenyezi-Mungu huwategemeza waadilifu.

Kusoma sura kamili Zaburi 37