Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 37:30-38 Biblia Habari Njema (BHN)

30. Mtu mwadilifu husema maneno ya hekima,kwa ulimi wake hunena yaliyo ya haki.

31. Huizingatia moyoni mwake sheria ya Mungu wake;naye hatetereki katika mwenendo wake.

32. Mtu mwovu humvizia mtu mwema na kujaribu kumuua;

33. lakini Mwenyezi-Mungu hatamtia mtu mwema makuchani mwake,wala kumwacha apatilizwe akishtakiwa.

34. Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kushika njia yake,naye atakukuza uimiliki nchi,na kuwaona waovu wakiangamizwa.

35. Nilimwona mwovu mdhalimu sana,alijiweka juu ya wote kama mierezi ya Lebanoni!

36. Baadaye nikapita hapo, naye hakuwapo tena;nikamtafuta, lakini hakuonekana tena.

37. Mwangalie mtu mwema, mtu mwadilifu;mtu anayependa amani hujaliwa wazawa.

38. Lakini wakosefu wote wataangamizwa;na wazawa wao watafutiliwa mbali.

Kusoma sura kamili Zaburi 37