29. Waadilifu wataimiliki nchi,na wataishi humo milele.
30. Mtu mwadilifu husema maneno ya hekima,kwa ulimi wake hunena yaliyo ya haki.
31. Huizingatia moyoni mwake sheria ya Mungu wake;naye hatetereki katika mwenendo wake.
32. Mtu mwovu humvizia mtu mwema na kujaribu kumuua;
33. lakini Mwenyezi-Mungu hatamtia mtu mwema makuchani mwake,wala kumwacha apatilizwe akishtakiwa.
34. Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kushika njia yake,naye atakukuza uimiliki nchi,na kuwaona waovu wakiangamizwa.
35. Nilimwona mwovu mdhalimu sana,alijiweka juu ya wote kama mierezi ya Lebanoni!
36. Baadaye nikapita hapo, naye hakuwapo tena;nikamtafuta, lakini hakuonekana tena.
37. Mwangalie mtu mwema, mtu mwadilifu;mtu anayependa amani hujaliwa wazawa.
38. Lakini wakosefu wote wataangamizwa;na wazawa wao watafutiliwa mbali.
39. Mwenyezi-Mungu huwaokoa waadilifu,na kuwalinda wakati wa taabu.
40. Mwenyezi-Mungu huwasaidia na kuwaokoa;huwatoa makuchani mwa waovu na kuwaokoa,maana wanakimbilia usalama kwake.