Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 37:18-30 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Mwenyezi-Mungu hutunza maisha ya watu waaminifu,na urithi wao utadumu milele.

19. Hawataaibika zikifika nyakati mbaya;siku za njaa watakuwa na chakula tele.

20. Lakini waovu wataangamia,maadui za Mwenyezi-Mungu watanyauka kama maua nyikani;naam, watatoweka kama moshi.

21. Mtu mwovu hukopa bila kurudisha;lakini mwadilifu hutoa kwa ukarimu.

22. Waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi,lakini waliolaaniwa naye watafutiliwa mbali.

23. Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu,humlinda yule ampendezaye.

24. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini,kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza.

25. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee;kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu,au watoto wake wakiombaomba chakula.

26. Daima huwapa wengine kwa furaha na kukopesha,na watoto wake ni baraka.

27. Achana na uovu, utende mema,nawe utaishi nchini daima;

28. maana Mwenyezi-Mungu hupenda uadilifu,wala hawaachi waaminifu wake.Huwalinda hao milele;lakini wazawa wa waovu wataangamizwa.

29. Waadilifu wataimiliki nchi,na wataishi humo milele.

30. Mtu mwadilifu husema maneno ya hekima,kwa ulimi wake hunena yaliyo ya haki.

Kusoma sura kamili Zaburi 37