Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 37:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Usihangaike kwa sababu ya waovu;usiwaonee wivu watendao mabaya.

2. Maana hao watatoweka mara kama nyasi;watanyauka kama mimea mibichi.

3. Mtumainie Mwenyezi-Mungu na kutenda mema,upate kuishi katika nchi na kuwa salama.

4. Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu,naye atakujalia unayotamani moyoni.

Kusoma sura kamili Zaburi 37