Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 35:8-14 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,wanaswe katika mtego wao wenyewe,watumbukie humo na kuangamia!

9. Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10. Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”

11. Mashahidi wakorofi wanajitokeza;wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12. Wananilipa mema yangu kwa mabaya;nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13. Lakini wao walipokuwa wagonjwa,mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;nilijitesa kwa kujinyima chakula.Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14. kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

Kusoma sura kamili Zaburi 35