Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 35:19-23 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20. Maneno wasemayo si ya amani,wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21. Wananishtaki kwa sauti:“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,usikae mbali nami.

23. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

Kusoma sura kamili Zaburi 35