Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 35:11-21 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mashahidi wakorofi wanajitokeza;wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12. Wananilipa mema yangu kwa mabaya;nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13. Lakini wao walipokuwa wagonjwa,mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;nilijitesa kwa kujinyima chakula.Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14. kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15. Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.Walikusanyika pamoja dhidi yangu.Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,wala hakuna aliyewazuia.

16. Watu ambao huwadhihaki vilema,walinisagia meno yao kwa chuki.

17. Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18. Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19. Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20. Maneno wasemayo si ya amani,wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21. Wananishtaki kwa sauti:“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

Kusoma sura kamili Zaburi 35