Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 35:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;uwashambulie hao wanaonishambulia.

2. Utwae ngao yako na kingio lako,uinuke uje ukanisaidie!

3. Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4. Waone haya na kuaibika,hao wanaoyanyemelea maisha yangu!Warudishwe nyuma kwa aibu,hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5. Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6. Njia yao iwe ya giza na utelezi,wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7. Maana walinitegea mitego bila sababu;walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8. Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,wanaswe katika mtego wao wenyewe,watumbukie humo na kuangamia!

9. Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10. Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”

11. Mashahidi wakorofi wanajitokeza;wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12. Wananilipa mema yangu kwa mabaya;nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

Kusoma sura kamili Zaburi 35