21. Asifiwe Mwenyezi-Mungu,maana amenionesha fadhili zake kwa namna ya ajabu,nilipozingirwa kama mji unaoshambuliwa.
22. Nami niliogopa na kudhani kwamba ulikuwa umenitupa;kumbe, ulisikia kilio changu nilipokuita unisaidie.
23. Mpendeni Mwenyezi-Mungu, enyi watakatifu wake wote.Mwenyezi-Mungu huwalinda watu waaminifu;lakini huwaadhibu kabisa wenye kiburi wanavyostahili.
24. Muwe hodari na kupiga moyo konde,enyi nyote mnaomtumainia Mwenyezi-Mungu.