Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 31:16-21 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Uniangalie kwa wema mimi mtumishi wako;uniokoe kwa fadhili zako.

17. Usiniache niaibike ee Mwenyezi-Mungu,maana mimi ninakuomba;lakini waache waovu waaibike,waache wapotelee kwa mshangao huko kuzimu.

18. Izibe midomo ya hao watu waongo,watu walio na kiburi na majivuno,ambao huwadharau watu waadilifu.

19. Jinsi gani ulivyo mwingi wema wako,uliowawekea wale wanaokucha!Wanaokimbilia usalama kwakowawapa mema binadamu wote wakiona.

20. Wawaficha mahali salama hapo ulipo,mbali na mipango mibaya ya watu;wawaweka salama katika ulinzi wako,mbali na ubishi wa maadui zao.

21. Asifiwe Mwenyezi-Mungu,maana amenionesha fadhili zake kwa namna ya ajabu,nilipozingirwa kama mji unaoshambuliwa.

Kusoma sura kamili Zaburi 31