Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 31:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kwako, ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama,usiniache niaibike kamwe;kwa uadilifu wako uniokoe.

2. Unitegee sikio, uniokoe haraka!Uwe kwangu mwamba wa usalama,ngome imara ya kuniokoa.

3. Naam, wewe ni mwamba wangu na ngome yangu;kwa hisani yako uniongoze na kunielekeza.

4. Unitoe katika mtego walionitegea mafichoni;maana wewe ni kimbilio la usalama wangu.

5. Mikononi mwako naiweka roho yangu;umenikomboa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu mwaminifu.

6. Wawachukia wanaoabudu sanamu batili;lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu.

7. Nitashangilia na kufurahia fadhili zako,maana wewe waiona dhiki yangu,wajua na taabu ya nafsi yangu.

8. Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu;umenisimamisha mahali pa usalama.

Kusoma sura kamili Zaburi 31