Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 28:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Uwaadhibu kadiri ya matendo yao,kufuatana na maovu waliyotenda.Waadhibu kadiri ya matendo yao wenyewe;uwatendee yale wanayostahili.

5. Hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu;hawatambui mambo aliyoyafanya.Kwa sababu hiyo atawabomoa,wala hatawajenga tena upya.

6. Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,maana amesikiliza ombi langu.

7. Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu;tegemeo la moyo wangu limo kwake.Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo;kwa wimbo wangu ninamshukuru.

8. Mwenyezi-Mungu ni nguvu ya watu wake;yeye ni kimbilio la wokovu kwa mfalme wake mteule.

9. Ee Mungu, uwaokoe watu wako;uwabariki watu hao walio mali yako.Uwe mchungaji wao na kuwategemeza milele.

Kusoma sura kamili Zaburi 28