Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 28:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu!Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi,la sivyo kama usiponisikiliza,nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.

2. Sikiliza sauti ya ombi langu,ninapokulilia unisaidie,ninapoinua mikono yangu kuelekea maskani yako takatifu.

3. Usinipatilize pamoja na watu wabaya,pamoja na watu watendao maovu:Watu wasemao na wenzao maneno ya amani,kumbe wamejaa uhasama moyoni.

4. Uwaadhibu kadiri ya matendo yao,kufuatana na maovu waliyotenda.Waadhibu kadiri ya matendo yao wenyewe;uwatendee yale wanayostahili.

5. Hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu;hawatambui mambo aliyoyafanya.Kwa sababu hiyo atawabomoa,wala hatawajenga tena upya.

6. Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,maana amesikiliza ombi langu.

Kusoma sura kamili Zaburi 28