Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 26:4-11 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Sijumuiki na watu wapotovu;sishirikiani na watu wanafiki.

5. Nachukia mikutano ya wabaya;wala sitajumuika na waovu.

6. Nanawa mikono yangu kuonesha sina hatia,na kuizunguka madhabahu yako, ee Mwenyezi-Mungu,

7. nikiimba wimbo wa shukrani,na kusimulia matendo yako yote ya ajabu.

8. Ee Mwenyezi-Mungu, napenda makao yako,mahali unapokaa utukufu wako.

9. Usiniangamize pamoja na wenye dhambi,wala usinitupe pamoja na wauaji,

10. watu ambao matendo yao ni maovu daima,watu ambao wamejaa rushwa.

11. Lakini mimi ninaishi kwa unyofu;unihurumie na kunikomboa.

Kusoma sura kamili Zaburi 26