Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 21:8-13 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mkono wako ewe mfalme utawakamata maadui zako wote;mkono wako wa kulia utawakamata wanaokuchukia.

9. Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto.Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake,moto utawateketeza kabisa.

10. Utawaangamiza wazawa wao kutoka duniani;watoto wao hawatasalia kati ya binadamu.

11. Hata kama wakipanga maovu dhidi yako,kama wakitunga mipango ya hila,kamwe hawataweza kufaulu.

12. Kwa maana wewe utawatimua mbio,utawalenga usoni kwa mishale yako.

13. Utukuzwe ee Mwenyezi-Mungu kwa sababu ya nguvu yako!Tutaimba na kuusifu uwezo wako.

Kusoma sura kamili Zaburi 21