Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 21:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako,anafurahi mno kwa msaada uliompa.

2. Umemtimizia matakwa ya moyo wake;wala hukumkatalia ombi lake.

3. Umemjia, ukampa baraka nzurinzuri;umemvika taji ya dhahabu safi kichwani mwake.

4. Alikuomba maisha nawe ukampa;ulimpa maisha marefu milele na milele.

5. Kwa msaada wako ametukuka sana;wewe umemjalia fahari na heshima.

6. Wamjalia baraka zako daima;wamfurahisha kwa kuwako kwako.

7. Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu;kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.

8. Mkono wako ewe mfalme utawakamata maadui zako wote;mkono wako wa kulia utawakamata wanaokuchukia.

9. Utakapotokea utawaangamiza kama kwa tanuri ya moto.Mwenyezi-Mungu atawamaliza kwa hasira yake,moto utawateketeza kabisa.

10. Utawaangamiza wazawa wao kutoka duniani;watoto wao hawatasalia kati ya binadamu.

11. Hata kama wakipanga maovu dhidi yako,kama wakitunga mipango ya hila,kamwe hawataweza kufaulu.

Kusoma sura kamili Zaburi 21