Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 20:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni;jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

2. Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake;akutegemeze kutoka mlima Siyoni.

3. Azikumbuke sadaka zako zote;azikubali tambiko zako za kuteketezwa.

4. Akujalie unayotamani moyoni mwako,aifanikishe mipango yako yote.

5. Tutashangilia kwa ajili ya ushindi wako;tutatweka bendera kulitukuza jina la Mungu wetu.Mwenyezi-Mungu akutimizie maombi yako yote!

6. Najua Mwenyezi-Mungu atamsaidia mfalme aliyemteua,atamjibu kutoka patakatifu pake mbinguni;kwa mkono wake wa kulia atamjalia ushindi mkubwa.

7. Wengine hujigamba kwa magari ya vita;wengine hujigamba kwa farasi wao.Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

Kusoma sura kamili Zaburi 20