Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 19:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu,humpa mtu uhai mpya;masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti,huwapa hekima wasio na makuu.

8. Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa,huufurahisha moyo;amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi,humwelimisha mtu.

9. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni jambo jema,na la kudumu milele;maagizo ya Mwenyezi-Mungu ni sawa,yote ni ya haki kabisa.

10. Yatamanika kuliko dhahabu;kuliko dhahabu safi kabisa.Ni matamu kuliko asali;kuliko asali safi kabisa.

11. Yanifunza mimi mtumishi wako;kuyafuata kwaniletea tuzo kubwa.

12. Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe?Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua.

13. Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi,usikubali hayo yanitawale.Hapo nitakuwa mkamilifu,wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

14. Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu,yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu,mwamba wangu na mkombozi wangu!

Kusoma sura kamili Zaburi 19