Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 19:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Hamna msemo au maneno yanayotumika;wala hakuna sauti inayosikika;

4. hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote,na maneno yao yafika kingo za ulimwengu.Mungu ameliwekea jua makao yake angani;

5. nalo hutoka kama bwana arusi chumbani mwake,lafurahi kama shujaa aliye tayari kushindana.

6. Lachomoza toka upande mmoja,na kuzunguka hadi upande mwingine;hakuna kiwezacho kuliepa joto lake.

Kusoma sura kamili Zaburi 19