13. Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni;Mungu Mkuu akatoa sauti yake,kukatokea mvua ya mawe na makaa ya moto.
14. Aliwapiga maadui mishale yake, akawatawanya,alirusha umeme, akawatimua.
15. Ulipowakemea maadui zako ee Mwenyezi-Mungu,ulipowatisha kwa ghadhabu yako,vilindi vya bahari vilifunuliwa,misingi ya dunia ikaonekana.
16. Mungu alinyosha mkono kutoka juu akanichukua,kutoka katika maji mengi alininyanyua.
17. Aliniokoa kutoka kwa maadui zangu wenye nguvu nyingi,aliniokoa kutoka kwa hao walionichukia,maana walikuwa na nguvu kunishinda.
18. Walinivamia nilipokuwa taabuni,lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.