1. Nakupenda, ee Mwenyezi-Mungu, nguvu yangu!
2. Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu,ngome yangu na mkombozi wangu;Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama;ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.
3. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.
4. Kamba za kifo zilinizingira,mawimbi ya maangamizi yalinivamia;
5. kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.
6. Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu,nilimlilia Mungu wangu anisaidie.Aliisikia sauti yangu hekaluni mwake;kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
7. Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika;misingi ya milima ikayumbayumba,kwani Mungu alikuwa amekasirika.
8. Moshi ulifuka kutoka puani mwake,moto uunguzao ukatoka kinywani mwake;makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.
9. Aliinamisha anga, akashuka chini;na wingu jeusi chini ya miguu yake.