Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 17:4-14 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kuhusu matendo watendayo watu;mimi nimeitii amri yako,nimeepa njia ya wadhalimu.

5. Nimefuata daima njia yako;wala sijateleza kamwe.

6. Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu;unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.

7. Onesha fadhili zako za ajabu,uwaokoe kutoka kwa adui zao,wale wanaokimbilia usalama kwako.

8. Unilinde kama mboni ya jicho;unifiche kivulini mwa mabawa yako,

9. mbali na mashambulio ya waovu,mbali na maadui zangu hatari wanaonizunguka.

10. Hao hawana huruma yoyote moyoni;wamejaa maneno ya kujigamba.

11. Wananifuatia na kunizunguka;wananivizia waniangushe chini.

12. Wako tayari kunirarua kama simba:Kama mwanasimba aviziavyo mawindo.

13. Inuka, ee Mwenyezi-Mungu,uwakabili na kuwaporomosha.Kwa upanga uiokoe nafsi yangu kutoka kwa waovu.

14. Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu,uniokoe mikononi mwa watu hao,watu ambao riziki yao ni dunia hii tu. Uwajaze adhabu uliyowawekea,wapate ya kuwatosha na watoto wao,wawaachie hata na wajukuu zao.

Kusoma sura kamili Zaburi 17