Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 16:4-11 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Lakini wanaoabudu miungu mingine,watapata mateso mengi.Tambiko ya damu sitaitolea kamwe,na majina ya miungu hiyo sitayataja.

5. Wewe ee Mwenyezi-Mungu ndiwe riziki yangu kuu,majaliwa yangu yamo mikononi mwako.

6. Umenipimia sehemu nzuri sana;naam, urithi wangu ni wa kupendeza.

7. Namsifu Mwenyezi-Mungu kwa kuniongoza,usiku dhamiri yangu yanionya.

8. Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima;yuko pamoja nami, wala sitatikisika.

9. Kwa hiyo nitafurahi kwa moyo wote na kushangilia,nami nitakaa salama salimini.

10. Naam wewe hutaiacha nafsi yangu kuzimu,hutaniacha mimi mwaminifu wako nipate kuoza.

11. Wanionesha njia ya kufikia uhai;kuwako kwako kwanijaza furaha kamili,katika mkono wako wa nguvu mna mema ya milele.

Kusoma sura kamili Zaburi 16