Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 15:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako?Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu?

2. Ni mtu aishiye bila lawama,atendaye daima yaliyo mema,asemaye ukweli kutoka moyoni;

3. ni mtu asiyesengenya watu,asiyemtendea uovu rafiki yake,wala kumfitini jirani yake;

4. ni mtu anayewadharau wafisadi,lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu;ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara;

5. asiyekopesha fedha yake kwa riba,wala kupokea rushwa kumdhulumu asiye na hatia.Mtu atendaye hayo,kamwe hatatikisika.

Kusoma sura kamili Zaburi 15