Agano la Kale

Agano Jipya

Zaburi 11:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama;mnawezaje basi kuniambia:“Ruka kama ndege, mpaka milimani,

2. maana waovu wanavuta pinde;wameweka mishale tayari juu ya uta,wawapige mshale watu wema gizani!

3. Kama misingi ikiharibiwa,mtu mwadilifu atafanya nini?”

4. Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu;kiti cha enzi cha Mwenyezi-Mungu kiko mbinguni.Kwa macho yake huwachungulia wanadamu,na kujua kila kitu wanachofanya.

5. Mwenyezi-Mungu huwapima waadilifu na waovu;huwachukia kabisa watu wakatili.

6. Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti;upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao.

7. Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu;watu wanyofu watakaa pamoja naye.

Kusoma sura kamili Zaburi 11