Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 19:10-27 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi.

11. Kutoka huko mpaka wake ulikwenda magharibi hadi Mareali, ukapitia pembeni mwa Dabeshethi na kwenda kwenye kijito kilichoko mashariki ya Yokneamu.

12. Kutoka Saridi, mpaka huo ulielekea mashariki hadi kwenye mpaka wa Kisloth-tabori, na kutoka huko ukapita Daberathi hadi Yafia.

13. Kutoka Yafia uliendelea mashariki hadi Gath-heferi, Eth-kasini, na kuendelea hadi Rimoni ambako ulipanda kuelekea Nea.

14. Upande wa kaskazini mpaka uligeuka kuelekea Hanathoni na kuishia kwenye bonde la Yiftaheli.

15. Ukajumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Yidala na Bethlehemu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake.

16. Hiyo ndiyo sehemu zilizopewa koo za kabila la Zebuluni miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

17. Kura ya nne ilizipata koo za kabila la Isakari.

18. Eneo lenyewe lilikuwa na miji ya Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,

19. Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,

20. Rabithi, Kishioni, Ebesi,

21. Remethi, En-ganimu, En-hada na Beth-pasesi.

22. Kadhalika, mpaka wao ulifika Tabori, Shahasuma, Beth-shemeshi na kuishia kwenye mto Yordani. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na sita pamoja na vijiji vyake.

23. Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Isakari; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

24. Kura ya tano ilizipata koo za kabila la Asheri.

25. Eneo la nchi yao lilikuwa na miji ya Helkathi, Hali, Beteni, Akshafi,

26. Alameleki, Amadi na Mishali. Kwa upande wa magharibi mpaka uligusana na Karmeli na Shihor-libnathi.

27. Kisha ukageuka kuelekea mashariki kwenda Beth-dagoni ambako unagusana na Zebuluni na bonde la Iftaheli. Halafu ukaendelea kaskazini hadi Beth-emeki, Neieli na kuzidi kuelekea kaskazini hadi Kabuli,

Kusoma sura kamili Yoshua 19