Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 19:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.

2. Kabila la Simeoni lilipata miji ya Beer-sheba, Sheba, Molada

3. Hasar-shuali, Bala, Esemu,

4. Eltoladi, Bethuli, Horma,

5. Siklagi, Beth-markabothi, Hasar-susa,

6. Beth-lebaothi na Sharuheni. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.

7. Pia kulikuwa na miji ya En-rimoni, Etheri, na Ashani. Jumla ya miji waliyopewa ni minne pamoja na vijiji vyake.

8. Pamoja na vijiji vyote vilivyoizunguka miji hiyo hadi Baalath-beeri, (au Rama) ya Negebu. Hizo zote ni sehemu zilizopewa koo za kabila la Simeoni.

9. Kwa vile eneo lililopewa kabila la Yuda lilikuwa kubwa kuliko kabila hilo lilivyohitaji, sehemu ya eneo lake lilipewa kabila la Simeoni.

10. Kura ya tatu ilizipata koo za kabila la Zebuluni. Eneo lao lilienea hadi Saridi.

11. Kutoka huko mpaka wake ulikwenda magharibi hadi Mareali, ukapitia pembeni mwa Dabeshethi na kwenda kwenye kijito kilichoko mashariki ya Yokneamu.

12. Kutoka Saridi, mpaka huo ulielekea mashariki hadi kwenye mpaka wa Kisloth-tabori, na kutoka huko ukapita Daberathi hadi Yafia.

Kusoma sura kamili Yoshua 19