Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24

Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 16 Biblia Habari Njema (BHN)

Nchi ya Efraimu na ya Manase

1. Sehemu waliyogawiwa wazawa wa Yosefu kwa kura ilianzia karibu na mto Yordani, mashariki ya chemchemi ya Yeriko, na kupitia jangwani, hadi kwenye sehemu za milima mpaka Betheli.

2. Kutoka Betheli mpaka ulielekea Luzu ukapita Atarothi ambako waliishi Waarki.

3. Kisha ukashuka magharibi katika nchi ya Wayafleti hadi Beth-horoni ya Chini na Gezeri na kuishia kwenye bahari ya Mediteranea.

4. Wazawa wa Yosefu, yaani kabila la Manase na kabila la Efraimu, walipewa nchi hiyo kuwa milki yao.

Nchi ya kabila la Efraimu

5. Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu,

6. na kuishia bahari ya Mediteranea. Kwa upande wa kaskazini mpaka ulipita Mikmethathi na kwa mashariki yake ulizunguka na kuelekea Taanath-shilo ambako ulipita upande wa mashariki hadi Yanoa.

7. Kutoka Yanoa ulikwenda hadi Atarothi na Naara, hata kufika Yeriko, ambako uliishia katika mto Yordani.

8. Kutoka Tapua, mpaka ulikwenda magharibi hadi kijito cha Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao,

9. pamoja na miji na vijiji ambavyo waliongezewa kutoka kwenye nchi ya kabila la Manase.

10. Waefraimu hawakuwafukuza Wakanaani walioishi Gezeri. Wakanaani hao waliendelea kukaa miongoni mwa watu wa Efraimu mpaka leo, wakiwa watumwa wa kuwafanyia kazi za kulazimishwa.