Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 15:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mpaka huo ukapita Bethi-hogla na kaskazini ya Beth-araba hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

7. Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.

8. Kisha, mpaka huo ulipitia kwenye Bonde la Hinomu, upande wa kusini mwa kilima cha Wayebusi, yaani Yerusalemu, kuelekea kilele cha mlima ulio magharibi ya bonde la Hinomu na kufika mwishoni mwa bonde la Refaimu.

9. Kutoka hapo, ulielekea mlimani hadi chemchemi za Neftoa, mpaka kwenye miji ya mlima wa Efroni. Hapo mpaka uligeuka na kuelekea Baala, yaani Kiriath-yearimu,

10. ambako ulipinda magharibi kuelekea Mlima Seiri; ukapita kaskazini ya mlima wa Yerimu, yaani Kesaloni, na kuteremka hadi Beth-shemeshi ambapo ulipita karibu na Timna.

11. Kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Ekroni, ukazunguka kuelekea Shikroni ambapo ulipita karibu na mlima Baala hadi Yabneeli ukaishia katika bahari ya Mediteranea.

Kusoma sura kamili Yoshua 15