Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 15:47-63 Biblia Habari Njema (BHN)

47. Ashdodi na Gaza pamoja na miji na vijiji vyake, mpaka kijito cha Misri hadi pwani ya bahari ya Mediteranea.

48. Miji iliyokuwa kwenye eneo la milimani ni Shamiri, Yatiri, Soko,

49. Dana, Kiriath-sana (yaani Debiri),

50. Anabu, Eshtemoa, Animu,

51. Gosheni, Holoni na Gilo. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.

52. Walipewa pia miji ya Arabu, Duma, Eshani,

53. Yanimu, Beth-tapua, Afeka,

54. Humta, Kiriath-arba (yaani Hebroni) na Siori. Jumla ya miji waliyopewa ni tisa pamoja na vijiji vyake.

55. Pia walipewa miji ya Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,

56. Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,

57. Kaini, Gibea na Timna. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi pamoja na vijiji vyake.

58. Vilevile miji ya Halhuli, Beth-suri, Gedori,

59. Maarathi, Beth-anothi na Eltekoni. Jumla ya miji waliyopewa ni sita pamoja na vijiji vyake.

60. Kadhalika walipewa Kiriath-baali, uitwao pia Kiriath-yearimu, na Raba. Jumla ya miji waliyopewa ni miwili pamoja na vijiji vyake.

61. Miji ya nyikani ilikuwa Beth-araba, Midini, Sekaka,

62. Nibshani, Mji wa Chumvi na Engedi. Jumla ya miji waliyopewa ni sita pamoja na vijiji vyake.

63. Lakini watu wa Yuda hawakuweza kuwafukuza Wayebusi, ambao ndio waliokuwa wenyeji wa Yerusalemu, na mpaka leo Wayebusi bado wanaishi mjini humo pamoja na watu wa Yuda.

Kusoma sura kamili Yoshua 15