Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 15:18-28 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Katika siku yao ya harusi, Aksa alimwambia Othnieli amwombe Kalebu shamba. Aksa alikuwa amepanda punda, na alipokuwa anashuka chini, Kalebu akamwuliza, “Unataka nikupe nini?”

19. Aksa akamjibu, “Nipe zawadi; nipe sehemu yenye maji kwa kuwa huko Negebu ulikonipa ni kukavu.” Basi, Kalebu akampa chemchemi za maji zilizokuwa kwenye nyanda za juu na za chini.

20. Hii ndiyo nchi waliyopewa watu wa kabila la Yuda kulingana na koo zake.

21. Miji iliyokuwa upande wa kusini kabisa wa nchi ya Yuda kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: Kabseeli, Ederi, Yaguri,

22. Kina, Dimona, Adada,

23. Kedeshi, Hazori, Ithnani,

24. Zifu, Telemu, Bealothi,

25. Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (yaani Hazori),

26. Amamu, Shema, Molada,

27. Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti,

28. Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia,

Kusoma sura kamili Yoshua 15