Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 15:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini.

2. Mpaka wao upande wa kusini ulianza pembe ya kusini ya Bahari ya Chumvi,

3. ukaendelea kusini hadi mwinuko wa Akrabimu, ukapitia kando ya Sini, na kusini ya Kadesh-barnea, ukipitia Hesroni hadi Adari na kisha ukageuka kuelekea Karka.

4. Kutoka hapo ulipita karibu na Asmoni na kufuata kijito cha Misri hadi kufikia kwenye bahari ya Mediteranea. Hapo ndipo ulipopita mpaka wa kusini wa Yuda.

5. Mpaka wao wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi hadi pale mto Yordani unapoingilia baharini. Na mpaka wao upande wa kaskazini ulipita kutoka pembe ya Bahari ya Chumvi mahali ambapo mto Yordani unaingilia baharini.

6. Mpaka huo ukapita Bethi-hogla na kaskazini ya Beth-araba hadi kwenye jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.

7. Kutoka hapo, uliendelea hadi Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, ulio karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko kusini mwa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemchemi za En-shemeshi na kuishia En-rogeli.

Kusoma sura kamili Yoshua 15