Agano la Kale

Agano Jipya

Yoshua 1:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya kifo cha Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mose:

2. “Mtumishi wangu Mose amefariki, sasa vukeni mto Yordani, wewe pamoja na Waisraeli wote hadi kwenye nchi ile ambayo ninawapa.

3. Kila mahali mtakapokanyaga nimewapeni kama nilivyomwahidi Mose.

4. Mipaka ya nchi yenu itakuwa hivi: Kusini ni jangwa, kaskazini ni milima ya Lebanoni, mashariki ni mto ule mkubwa Eufrate, kupitia nchi yote ya Wahiti hadi bahari ya Mediteranea upande wa magharibi.

Kusoma sura kamili Yoshua 1