Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 1:8-18 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Lieni kama msichana aliyevaa vazi la guniaakiombolezea kifo cha mchumba wake.

9. Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.Makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, wanaomboleza.

10. Mashamba yamebaki matupu;nchi inaomboleza,maana nafaka imeharibiwa,divai imetoweka,mafuta yamekosekana.

11. Ombolezeni enyi wakulima;pigeni yowe enyi watunza mizabibu.Ngano na shayiri zimeharibika,mavuno yote shambani yameangamia.

12. Mizabibu imenyauka;mitini imedhoofika;mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka,naam miti yote shambani imekauka.Furaha imetoweka miongoni mwa watu.

13. Enyi makuhani, jivikeni magunia kuomboleza,lieni enyi wahudumu wa madhabahu.Ingieni hekaluni mkaomboleze usiku kucha!Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mungu.

14. Toeni amri watu wafunge;itisheni mkutano wa kidini.Kusanyeni wazee na wakazi wote wa nchi,nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,na humo mkamlilie Mwenyezi-Mungu.

15. Ole wetu kwa ile siku ya Mwenyezi-Mungu,siku hiyo ya Mwenyezi-Mungu inakaribia;inakuja pamoja na maangamizi,kutoka kwa Mungu Mkuu.

16. Mazao yetu yameharibiwa huku tunatazama.Furaha na kicheko vimetoweka nyumbani kwa Mungu wetu.

17. Mbegu zinaoza udongoni;ghala za nafaka ni ukiwa mtupu,ghala zimeharibika,kwa kukosa nafaka ya kuhifadhi.

18. Tazama wanyama wanavyolia kwa huzuni!Makundi ya ng'ombe yanahangaika,kwa sababu yamekosa malisho;hata makundi ya kondoo yanateseka.

Kusoma sura kamili Yoeli 1