Agano la Kale

Agano Jipya

Yoeli 1:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Nzige, makundi kwa makundi, wameivamia mimea;kilichoachwa na nzige kimeliwa na tunutu,kilichoachwa na tunutu kimeliwa na parare,kilichoachwa na parare kimeliwa na matumatu.

5. Enyi walevi, levukeni na kulia;pigeni yowe, enyi walevi wa divai;zabibu zote za kutengeneza divai mpya zimeharibiwa.

6. Jeshi la nzige limeivamia nchi yetu;lina nguvu na ni kubwa ajabu;meno yake ni kama ya simba,na magego yake ni kama ya simba jike.

7. Limeiharibu mizabibu yetu,na kuitafuna mitini yetu.Limeyabambua magamba yake na kuyatupa chini,na matawi yake yameachwa meupe.

8. Lieni kama msichana aliyevaa vazi la guniaakiombolezea kifo cha mchumba wake.

9. Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu.Makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, wanaomboleza.

Kusoma sura kamili Yoeli 1