Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 9:30-35 Biblia Habari Njema (BHN)

30. Hata kama nikitawadha kwa theluji,na kujitakasa mikono kwa sabuni,

31. hata hivyo, atanitumbukiza shimoni kwenye uchafu,na mavazi yangu yataniona kuwa kinyaa.

32. Mungu si mtu kama mimi niweze kumjibu,hata tuweze kwenda mahakamani pamoja.

33. Hakuna msuluhishi kati yetu,ambaye angeamua kati yetu sisi wawili.

34. Mungu na aniondolee hiyo fimbo ya kunipiga,na kitisho chake kisinitie hofu!

35. Hapo ningeweza kusema bila kumwogopa;kwani sivyo nilivyo nafsini mwangu.

Kusoma sura kamili Yobu 9