Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 9:17-28 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Yeye huniponda kwa dhoruba;huongeza majeraha yangu bila sababu.

18. Haniachi hata nipumue;maisha yangu huyajaza uchungu.

19. Kama ni kushindana, yeye ana nguvu mno!Na kama ni kutafuta juu ya haki,nani atakayemleta mahakamani?

20. Ingawa sina hatia, maneno yangu yenyewe yangenihukumu;ingawa sina lawama, angenithibitisha kuwa mpotovu.

21. Sina lawama, lakini sijithamini.Nayachukia maisha yangu.

22. Yote ni mamoja, kwa hiyo nasema;Mungu huwaangamiza wema na waovu.

23. Maafa yaletapo kifo cha ghafla,huchekelea balaa la wasio na hatia.

24. Nchi ikitiwa watu waovu katika utawala wa mwovu,Mungu huyafumba macho ya mahakimu wake!Kama si yeye afanyaye hivyo, ni nani basi?

25. “Siku zangu zaenda mbio kuliko mpiga mbio;zinakimbia bila kuona faida.

26. Zapita kasi kama mashua ya matete;kama tai anayerukia mawindo yake.

27. Nasema: ‘Nitasahau lalamiko langu,niondoe uso wangu wa huzuni na kuwa na furaha!’

28. Lakini nayaogopa maumivu yangu yote,kwani najua Mungu hataniona kuwa sina hatia.

Kusoma sura kamili Yobu 9