Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 9:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka,mambo ya ajabu yasiyo na idadi.

11. Loo! Hupita karibu nami nisimwone,kisha huenda zake bila ya mimi kumtambua.

12. Tazama! Yeye huchukua anachotaka;nani awezaye kumzuia?Nani awezaye kumwuliza: ‘Unafanya nini?’

13. “Mungu hatazuia hasira yake;chini yake wainama kwa hofu Rahabu na wasaidizi wake.

14. Nitawezaje basi kumjibu Mungu?Nitachagua wapi maneno ya kumwambia?

15. Ingawa sina hatia, siwezi kumjibu.Lazima kumwomba anihurumie huyo mshtaki wangu.

16. Hata kama ningemwita naye akajibu,nisingeweza kuamini kuwa ananisikiliza.

17. Yeye huniponda kwa dhoruba;huongeza majeraha yangu bila sababu.

Kusoma sura kamili Yobu 9