Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 9:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha Yobu akajibu:

2. “Kweli najua hivyo ndivyo ilivyo.Lakini mtu awezaje kuwa mwema mbele ya Mungu?

3. Kama mtu angethubutu kushindana naye,hataweza kufika mbali;hata kujibu swali moja kati ya elfu.

4. Yeye ni mwenye hekima mno na nguvu nyingi,nani aliyepingana naye, akashinda?

5. Yeye huiondoa milima bila yenyewe kutambua,huibomolea mbali kwa hasira yake.

6. Yeye huitikisa dunia kutoka mahali pake,na nguzo zake zikatetemeka.

7. Huliamuru jua lisichomozehuziziba nyota zisiangaze.

8. Yeye peke yake alizitandaza mbingu,na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.

9. Ndiye aliyezifanya nyota angani:Dubu, Orioni, Kilimia, na nyota za kusini.

10. Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka,mambo ya ajabu yasiyo na idadi.

11. Loo! Hupita karibu nami nisimwone,kisha huenda zake bila ya mimi kumtambua.

12. Tazama! Yeye huchukua anachotaka;nani awezaye kumzuia?Nani awezaye kumwuliza: ‘Unafanya nini?’

Kusoma sura kamili Yobu 9