Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 8:15-21 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Wanaegemea nyumba yao lakini haitasimama,huishikilia lakini haidumu.

16. Jua litokapo yeye hustawi;hueneza matawi yake bustanini mwake.

17. Mizizi yake hujisokotasokota kwenye mawenaye aenda kuchunguza ndani ya mwamba.

18. Lakini akiangamizwa kutoka makao yake,hayo yatamkana yakisema: ‘Sijapata kukuona.’

19. Tazama, huo ndio mwisho wa furaha ya mtu huyo,na mahali pao patachipua wengine.

20. “Tazama! Mungu hatamkataa mtu asiye na hatia,wala kuwasaidia waovu.

21. Ila atakijaza kinywa chako kicheko,na midomo yako sauti ya furaha.

Kusoma sura kamili Yobu 8