Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 8:12-18 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Hata kama yamechanua na bila kukatwa,yakikosa maji hunyauka kabla ya mimea mingine.

13. Ndivyo walivyo wote wanaomsahau Mungu.Tumaini la wasiomwamini Mungu litapotea.

14. Tegemeo lao huvunjikavunjika,tumaini lao ni utando wa buibui.

15. Wanaegemea nyumba yao lakini haitasimama,huishikilia lakini haidumu.

16. Jua litokapo yeye hustawi;hueneza matawi yake bustanini mwake.

17. Mizizi yake hujisokotasokota kwenye mawenaye aenda kuchunguza ndani ya mwamba.

18. Lakini akiangamizwa kutoka makao yake,hayo yatamkana yakisema: ‘Sijapata kukuona.’

Kusoma sura kamili Yobu 8