Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 8:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ndipo Bildadi, Mshuhi, akamjibu Yobu:

2. “Utasema mambo haya mpaka lini?Mpaka lini maneno yako yatakuwa matupu kama upepo?

3. Kwani, wadhani Mungu hupotosha haki?Au, je, Mungu Mwenye Nguvu hupotosha ukweli?

4. Kama watoto wako wamemkosea Mungu,yeye amewalipiza matokeo ya uhalifu wao.

5. Kama utamtafuta Munguukamsihi huyo Mungu mwenye nguvu,

6. kama wewe u safi moyoni na mnyofu,kweli Mungu atakuja kukusaidia,na kukujalia makao unayostahili.

7. Na ingawa ulianza kuishi kwa unyongemaisha yako ya baadaye yatakuwa ya fahari zaidi.

Kusoma sura kamili Yobu 8