Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 8:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ndipo Bildadi, Mshuhi, akamjibu Yobu:

2. “Utasema mambo haya mpaka lini?Mpaka lini maneno yako yatakuwa matupu kama upepo?

3. Kwani, wadhani Mungu hupotosha haki?Au, je, Mungu Mwenye Nguvu hupotosha ukweli?

4. Kama watoto wako wamemkosea Mungu,yeye amewalipiza matokeo ya uhalifu wao.

5. Kama utamtafuta Munguukamsihi huyo Mungu mwenye nguvu,

6. kama wewe u safi moyoni na mnyofu,kweli Mungu atakuja kukusaidia,na kukujalia makao unayostahili.

7. Na ingawa ulianza kuishi kwa unyongemaisha yako ya baadaye yatakuwa ya fahari zaidi.

8. Jifunze tafadhali kwa wale waliotutangulia,zingatia mambo waliyogundua hao wazee.

9. Sisi ni watu wa juzijuzi tu, hatujui kitu;siku zetu duniani ni kivuli kipitacho.

10. Lakini wao watakufunza na kukuambia,mambo waliyopata kuyatoa katika maarifa yao:

11. Mafunjo huota tu penye majimaji,matete hustawi mahali palipo na maji.

12. Hata kama yamechanua na bila kukatwa,yakikosa maji hunyauka kabla ya mimea mingine.

Kusoma sura kamili Yobu 8