Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 7:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Binadamu anayo magumu duniani,na siku zake ni kama siku za kibarua!

2. Yeye ni kama mtumwa atamaniye kivuli,kama mwajiriwa angojaye kwa hamu mshahara wake.

3. Basi nimepangiwa miezi na miezi ya ubatili,yangu ni majonzi usiku hata usiku.

4. Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’Kwani saa za usiku huwa ndefu sana;nagaagaa kitandani mpaka kuche!

5. Mwili wangu umejaa mabuu na uchafu;ngozi yangu imekauka na kutokwa na usaha wa jipu.

6. Siku zangu zapita kasi kuliko gurudumu la mshonaji,nazo zafikia mwisho wake bila matumaini.

7. “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu;jicho langu halitaona jema lolote tena.

8. Anayeniona sasa, hataniona tena,punde tu ukinitazama nitakuwa nimetoweka.

9. Kama wingu lififiavyo na kutowekandivyo nao watu washukavyo kuzimu bila kurudi.

10. Anayeondoka harudi tena kwa jamaa yake,na pale alipokuwa anaishi husahaulika mara.

11. “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea;nitasema kwa msongo wa roho yangu,nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu.

Kusoma sura kamili Yobu 7