Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 6:26-30 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Je, mnadhani kwamba mwaweza kuyakosoa maneno?Maneno ya mtu aliyekata tamaa ni upepo tu.

27. Nyinyi mnathubutu hata kuwapigia yatima kura;mnawapigia bei hata marafiki zenu!

28. Lakini sasa niangalieni tafadhali.Mimi sitasema uongo mbele yenu.

29. Acheni tafadhali, kusiwe na uovu;acheni sasa, kwani mimi ni mnyofu.

30. Je, mnadhani kwamba nimesema uovu?Je, mnafikiri mimi siyatambui machungu?

Kusoma sura kamili Yobu 6