Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 6:10-21 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Hiyo ingekuwa faraja yangu,ningefurahi katika maumivu yasiyo na huruma.

11. Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea;sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.

12. Je, nguvu zangu ni kama za mawe?Au mwili wangu kama shaba?

13. Kweli kwangu hamna cha kunisaidia;msaada wowote umeondolewa kwangu.

14. “Anayekataa kumhurumia rafiki yake,anakataa kumcha Mungu mwenye nguvu.

15. Rafiki zangu wamenidanganya kama kijito,wamenihadaa kama mitaro isiyo na maji.

16. Ambayo imejaa barafu,na theluji imejificha ndani yake.

17. Lakini wakati wa joto hutoweka,wakati wa hari hubaki mito mikavu.

18. Misafara hupotea njia wakitafuta maji,hupanda nyikani na kufia huko.

19. Misafara ya Tema hutafuta tafuta,wasafiri wa Sheba hutumaini.

20. Huchukizwa kwa kutumaini bure,hufika kwenye vijito hivyo na kuudhika.

21. Nyinyi mmekuwa kama vijito hivyo,mwaona balaa yangu na kuogopa.

Kusoma sura kamili Yobu 6