Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 6:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yobu akamjibu Elifazi:

2. “Laiti mahangaiko yangu yangepimwa uzani wake,mateso yangu yote yakawekwa katika mizani!

3. Yangekuwa mazito kuliko mchanga wa pwani.Ndio maana maneno yangu ni ya kuropoka!

4. Naam, mishale ya Mungu Mwenye Nguvu imenichoma;nafsi yangu imekunywa sumu yake.Vitisho vya Mungu vimenikabili.

5. Je, pundamwitu hulia akiwa na majani,au ng'ombe akiwa na malisho?

6. Je, kitu kisicho na ladha chaweza kuliwa bila chumvi?Je ute wa yai una utamu wowote?

7. Sina hamu ya kuvigusa vyakula hivyo,hivyo ni vyakula vyangu vichukizavyo.”

8. “Laiti ningejaliwa ombi langu,Mungu akanipatia kile ninachotamani:

9. Kwamba angekuwa radhi kunipondaponda,angenyosha mkono wake anikatilie mbali!

10. Hiyo ingekuwa faraja yangu,ningefurahi katika maumivu yasiyo na huruma.

11. Lakini sina nguvu ya kuweza kuendelea;sijui mwisho wangu utakuwaje, nipate kuvumilia.

Kusoma sura kamili Yobu 6