Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 5:9-19 Biblia Habari Njema (BHN)

9. yeye atendaye makuu yasiyochunguzika,atendaye maajabu yasiyohesabika.

10. Huinyeshea nchi mvua,hupeleka maji mashambani.

11. Huwainua juu walio wanyonge,wenye kuomboleza huwapa usalama.

12. Huvunja mipango ya wenye hila,matendo yao yasipate mafanikio.

13. Huwanasa wenye hekima kwa werevu wao,mipango ya wajanja huikomesha mara moja.

14. Hao huona giza wakati wa mchana,adhuhuri hupapasapapasa kama vile usiku.

15. Lakini Mungu huwaokoa yatima wasiuawe,huwanyakua fukara mikononi mwa wenye nguvu.

16. Hivyo maskini wanalo tumaini,nao udhalimu hukomeshwa.

17. “Heri mtu yule ambaye Mungu anamrudi!Hivyo usidharau Mungu Mwenye Nguvu anapokuadhibu.

18. Kwani yeye huumiza na pia huuguza;hujeruhi, na kwa mkono wake huponya.

19. Atakuokoa katika maafa zaidi ya mara moja;katika balaa la mwisho, uovu hautakugusa.

Kusoma sura kamili Yobu 5