Agano la Kale

Agano Jipya

Yobu 5:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mazao yake huliwa na wenye njaa,hata nafaka iliyoota kati ya miiba;wenye tamaa huuonea shauku utajiri wake.

6. Kwa kawaida mateso hayatoki mavumbiniwala matatizo hayachipui udongoni.

7. Bali binadamu huzaliwa apate taabu,kama cheche za moto zirukavyo juu.

8. “Kama ningekuwa wewe ningemgeukia Mungu,ningemwekea yeye Mungu kisa changu,

9. yeye atendaye makuu yasiyochunguzika,atendaye maajabu yasiyohesabika.

10. Huinyeshea nchi mvua,hupeleka maji mashambani.

11. Huwainua juu walio wanyonge,wenye kuomboleza huwapa usalama.

12. Huvunja mipango ya wenye hila,matendo yao yasipate mafanikio.

Kusoma sura kamili Yobu 5